1 John 4:7-12

7 aWapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 8 bYeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo. 9 cHivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. 10 dHili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. 11 eMarafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. 12 fHakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote.Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

Copyright information for SwhKC